Kongamano hilo limeandaliwa na Jumuiya ya Wamiliki wa Viwanda na Wafanyabiashara Huru wa Uturuki MUSIAD.
Kwa mujibu wa gazeti la Zaman la nchini Uturuki, kongamano hilo litawajumuisha zaidi ya wamiliki wa viwanda na wafanyabiasha 3000 kutoka nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu. Kongamano hilo linahesabiwa kuwa muhimu zaidi la wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara wa nchi za Kiislamu.
Kongamano hilo linachukuliwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa kutilia maanani kwamba linajadili kwa kina masuala na changamoto muhimu zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu katika mtazamo wa biashara na uchumi.
Njia za kukabiliana na kudorora uchumi pamoja na uimarishaji wa benki za Kiislamu zitachunguzwa katika kongamano hilo. Vilevile umuhimu na nafasi ya teknolojia ya kisasa katika kuimarisha nafasi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC na mbinu za kuimarisha viwanda kwa shabaha ya kustawisha hali ya uchumi ya nchi hizo zitapewa umuhimu katika kongamano hilo. 660600