IQNA

11:58 - September 26, 2010
Habari ID: 2001495

Mawakili wa Misri wataka kukamatwa kwa kasisi aliyedharau Qur'ani

Mawakili wa Misri wametoa taarifa rasmi wakimtaka Abdul Majid Mahmoud mwendesha mashtaka mkuu wa nchi hiyo kutoa amri ya kutiwa nguvuni Deir Al Anba Bishoy kasisi wa Kikritso wa Misri ambaye ametoa matamshi ya kuikosea heshima Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa gazeti la Misri la as-Sharouq mawakili hao wametaka kasisi huyo atiwe nguvuni kwa kutoa matamshi yanayokejeli matukufu ya dini za mbinguni na kutoa madai ya kuwepo mambo yaliyopotoshwa katika Qur'ani. Wamesema kuwa kasisi huyo kwa muda sasa amekuwa akitoa matamshi ambayo yanalenga kuzusha fitina na mgawanyiko miongoni mwa Waislamu na Wakristo wa Misri.
Inasemekana kuwa katika hotuba yake aliyotoa wiki iliyopita huko Cyprus, Kasisi Bishoy alidai kuwa kuna aya moja iliyoongezwa kwenye Qur'ani baada ya kuaga dunia Mtume Mtukufu (saw) na katika utawala wa khalifa wa tatu, aya ambayo amesisitiza inapasa kufutwa.
Wakati huohuo, Papa Shenouda III, kiongozi wa Makopti wa Misri, Ahmad Tayyib, Sheikh wa al-Azhar na maulama pamoja na wanafikra wa Kuwait wamelaani matamshi ya kasisi huyo. Katika upande wa pili, Baraza Kuu la Masuala ya Kiislamu la Misri lilifanya kikao cha dharura hapo jana Jumamosi kwa lengo la kujadili suala hilo. 662439
captcha