IQNA

13:48 - September 27, 2010
Habari ID: 2002187

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiislamu walaani siasa za utawala wa Kizayuni

Katika taarifa yao ya mwisho ya kikao cha New York, Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC wamelaani siasa za ukandamizaji za utawala haramu wa Israel.

Kikao hicho ambacho pia kimehudhuriwa na Ekmeleddin Ihsanoghu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu, kimejadili kwa kina masuala na changamoto zinazoukabili ulimwengu wa Kiislamu na hasa suala la Ukanda wa Gaza na kuzingirwa kwake na utawala haramu wa Israel ambapo kimelaani vikali siasa za ukandamizaji za utawala huo dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.
Katika taarifa hiyo, mawaziri hao wamesisitiza udharura wa kuchunguzwa hujuma ya makomando wa utawala haramu wa Israel dhidi ya msafara wa meli za misaada ya kibinadamu kwa watu wa Gaza.
Wamekemea vikali kitendo hicho na kutaka Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu duniani kufanya kila liwezekanalo ili kupata chanzo na sababu za kushambuliwa kijeshi msafara huo. 663187
captcha