Gazeti la ad-Dastur la Jordan limeandika kuwa jumuiya hiyo imesema hatua ya Kasisi Bishoy ya kushuku itibari ya aya moja ya Qur'ani na kutaka ifutwe ni dharau ya wazi kwa Waislamu na pia hujuma dhidi ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Jumuiya ya Kimataifa ya Fiqhi ya Kiislamu imesema katika taarifa hiyo kwamba, matamshi kama hayo hutolewa tu na watu walio na historia ya chuki dhidi ya Qur'ani, Uislamu, Waislamu na wanadamu wote kwa ujumla.
Jumuiya hiyo ambayo imesema ni msemaji wa wanazuoni wa Kiislamu wa jamii za Kiislamu katika nchi za Mashariki na Magharibi, imelaani vikali madai, fikra na vitendo vya aina hiyo.
Tunakumbusha hapa kuwa hivi karibuni akihutubia mkutano wa kidini huko Cyprus, Kasisi Bishoy alitoa madai ya uongo kwamba kuna aya moja iliyozidishwa katika Qur'ani Tukufu baada ya kuaga dunia Mtume Mtukufu (saw) na katika kipindi cha utawala wa khalifa wa tatu, aya ambayo alitaka ifutwe. Matamshi hayo ya kuikosea heshima Qur'ani yameamsha hasira ya Waislamu duniani, ambao wametaka achukuliwe hatua za kisheria. 666477