IQNA

Mkutano wa kila mwaka wa Baraza la Ushirikiano wa Kiislamu na Marekani

16:58 - October 10, 2010
Habari ID: 2010098
Mkutano wa 16 wa kila mwaka wa Baraza la Ushirikiano wa Kiislamu na Marekani ulifanyika jana Jumamosi tarehe 9 Oktoba huko Arlington Virginia.
Mamia ya viongozi wa kidini na wawakilishi wa mashirika pamoja na jumuiya mbalimbali za Kiislamu za Marekani walishiriki katika kikao hicho.
Robert Beebe, mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Chicago, Shariff al-Jamal, mwanadamizi wa mradi wa kujengwa msikiti mkuu wa New York, Helen Thomas, mwandishi wa Marekani aliyelazimishwa kujiuzulu kazi yake huko White House kutokana na matamshi aliyotoa dhidi ya Wazayuni na Tariq Ramadhan mwanafikra wa Kiislamu ni baadhi ya watu waliohutubu katika mkutano huo.
Mkutano huo wa siku moja uliofanyika kwa lengo la kutoa mafunzo ya uongozi bora kwa Waislamu pia ulijadili masuala mengine yakiwemo ya utoaji hutuba mbele ya umma, mahojiano na vyombo vya habari, kuchunguza chuki dhidi ya Uislamu na kufahamu haki za kisheria.
Baraza la Uhusiano wa Kiislamu na Marekani ni jumuiya kubwa zaidi inayotetea haki za kiraia za Waislamu nchini Marekani.
Baraza hilo pia linashughulikia kueneza Uislamu nchini Marekani, kuimarisha mazungumzo kati ya dini tofauti, kutetea uhuru wa raia na kuimarisha nafasi ya Waislamu nchini humo. 671256
captcha