IQNA

23:22 - October 10, 2010
Habari ID: 2010192

Waislamu wa Kosovo waandamana kupinga marufuku ya hijabu

Maelfu ya Waislamu wa Kosovo wameandamana wakipinga marufuku ya vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu hijabu katika shule za nchi hiyo.

Waandamanaji ambao wengi wao walikuwa Waislamu walitoa nara dhidi ya serikali ya Kosovo na kuelekea kwenye majengo ya serikali katika mji wa Prishtina.
Waandamanaji hao walipiga nara za “simamisheni marufuku ya vazi la hijabu”, “ondoeni hijabu ya akili na si ya vichwa” na “jamhuri ya kidemokrasia ndiyo, na hapana kwa udikteta dhidi ya Uislamu”.
Japokuwa sheria za Kosovo zinatetea uhuru wa dini lakini viongozi wa sekta ya elimu ya nchi hiyo wamepiga marufuku nembo za kidini ikiwa ni pamoja na vazi la hijabu katika shule za nchi hiyo.
Siku chache zilizopita mtoto wa kike mwenye umri wa mika 16 alifukuzwa shuleni kwa sababu tu ya kuwa na vazi la hijabu.
Karibu asilimia 90 ya jamii ya watu milioni mbili wa Kosovo ni Waislamu. 671384
captcha