Kikao hicho kinahudhuriwa na wawakilishi wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la nchi za Kiislamu ISESCO na wanachama wa Kamati ya Habari la Masuala ya Utamaduni ya OIC.
Sherehe za kufunguliwa rasmi kikao hicho zimehudhuriwa na Rais Abdoulaye Wade wa Senegal ambaye pia ni mwenyekiti wa sasa wa OIC.
Kamati ya Habari la Masuala ya Utamaduni ya OIC ilianzishwa kwa lengo la kustawisha uhusiano kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu na imekuwa na mchango mkubwa katika kuendeeleza utamaduni na thamani za Kiislamu.
Mkuu wa uhusiano wa kigeni wa ISESCO Muhammad Gambari atawasilisha ripoti katika kikao hicho kuhusu shughuli za shirika hilo katika nyanja za mazungumzo kati ya dini mbalimbali, juhudi za kujenga uhusiano mwema kati ya watu, kukabiliana na njama za vyombo vya habari dhidi ya Uislamu na kulinda Quds Tukufu na utambulisho wa Kiislamu wa Palestina. 673451