IQNA

12:55 - October 14, 2010
Habari ID: 2012665

Ufaransa mwenyeji wa kikao cha wanafikra wa Kiislamu tokea karne ya 8 hadi 17 Miladia

Kikao cha 'wanafikra wa Kiislamu tokea karne ya 8 hadi 17 Miladia na mchango wao katika elimu ya kisasa, kimepangwa kufanyika Jumapili tarehe 24 Oktoba katika mji wa Nontr nchini Ufaransa.

Kwa mujibu wa Salamchatou kikao hicho kinafanyika kwa mnasaba wa kutajwa mwaka huu wa 2010 na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO kuwa mwaka wa kimataifa wa kukurubisha pamoja tamaduni.
Kikao hicho kinafanyika kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kiislamu ya Salam Shatou, Taasisi ya Ulimwengu wa Kiarabu na Jumuiya ya Sharki ya mji wa Nontr.
Wahadhiri wa Kiislamu wa vyuo vikuu vya Ufaransa watashiriki katika kikao hicho na kutoa hotuba kuhusiana na elimu ya kisasa na mchango wa Waislamu katika kuieneza.
Warsha za masomo na mashindano maalumu ya watoto na vijana ni baadhi ya ratiba zitakazotekelezwa pambizoni mwa kikao hicho cha kielimu na Kiislamu.
Vilevile Taasisi ya Ulimwengu wa Kiislamu itaendesha maonyesho ya masomo ya Kiarabu katika kikao hicho. 674401
captcha