Akizungumza mbele ya wanafunzi wa chuo hicho huko Cairo, Sheikh al-Tayyib amesema kuwa jukumu muhimu la taasisi hiyo katika zama hizi nyeti ni kuwabainishia walimwengu misingi na mafundisho sahihi ya Uislamu yakiwemo ya kuvumiliana pamoja na kupambana na fitina na tuhuma zisizo na msingi zinazotolewa dhidi ya Uislamu.
Amewataka wanafunzi wa al-Azhar kuzingatia maadili ya Kiislamu na kufanya juhudi za kueneza mafundisho sahihi ya Uislamu kwa kutumia mbinu na misimamo ya wastani huku wakivumilia majukumu ya kutetea thamani za Kiislamu. Amewataka pia wadumishe mawasiliano yao na vyuo vikuu kupitia Jumuiya ya Kimataifa ya Wanafunzi wa al-Azhar. 675294