Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, zaidi ya viongozi 40 wa jamii ya Waislamu mjini New York wameshiriki katika hafla ya kuanza 'Wiki ya Kufungua Milango ya Misikiti kwa Wasio Waislamu'. Hafla hiyo imefanyika katika Msikiti wa Taqwa mjini humo.
Al Amin Abdul Latifa mmoja kati ya wanachama wa Baraza la Uongozi wa Kiislamu mjini New York amesema, 'chanzo cha chuki dhidi ya Uislamu ni kutokuwepo ujuzi wa kutosha kuhusu dini ya Kiislamu. Wakati watu wanapokuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu Uislamu wanashangaa na kubadilisha mitazamo yao potofu'.
678657