Akizungumza katika Baraza la Makasisi wa Mashariki ya Kati huko Vatican, Kasisi Bostorz amesisitiza kwamba utawala huo hauwezi kutegemea ibara hiyo katika kuhalalisha hatua yake ya kuwahamishia Mayahudi katika ardhi za Wapalestina na kuwafukuza Wapalestina kutoka kwenye ardhi hizo. Amesema, aya za kitabu kitakatifu na mitazamo ya kidini ya Mayahudi haipasi kutumiwa kwa madhumuni ya kueneza dhulma duniani.
Katika sehemu nyingine ya maneno yake, Kasisi Bostorz amesema kuwa ibara iliyotajwa haina maana tena kwa mtazamo wa Wakristo kwa sababu ibara hiyo ilitumika katika Agano la Kale na kwamba baada ya kudhihiri ujumbe wa Nabii Isah (as) ibara hiyo haikuwa na maana tena kwa sababu ardhi iliyoahidiwa iligeuka na kuwa ardhi yote ya Mwenyezi Mungu.
Ameendelea kusema ardhi hiyo iligeuka na kuwa ardhi ya upendo, mapenzi, urafiki, uadilifu na usawa na kwamba watu wote katika ardhi hizo wanapasa kutii amri ya Mwenyezi Mungu.
Salim Bostorz amekosoa utumiaji Mayahudi na Wazayuni ibara kama vile 'kaumu iliyo bora' au 'watu wateule' na kusisitiza kwamba hakuna kaumu yoyote iliyo bora kuliko nyingine bali watu wote duniani ni sawa kuhusiana na thamani za kiutu na kwamba wote ni wateule wa Mwenyezi Mungu. 680966