IQNA

Masomo ya Qur'ani ya wafanyakazi wa jeshi la Yemen yameanza

17:35 - October 24, 2010
Habari ID: 2018829
Mafunzo ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu makhsusi kwa wafanyakazi wa jeshi la Yemen yalianza jana katika msikiti wa al Saleh katika mji wa Sanaa.
Masomo hayo yanasimamiwa na Idara ya Mwongozo wa Masuala ya Kiroho ya Jeshi la Yemen ikishirikiana na Akademia ya Kuhifadhi Qur'ani ya al Wajiin. Watu 100 wanashiriki katika masomo hayo yatakaoendelea kwa kipindi cha siku 15.
Mkurugenzi wa Idara ya Mwongozo wa Masuala ya Kiroho ya Jeshi la Yemen Ali Hassan al Shatir amesema kuwa masomo hayo yanatolewa kwa lengo la kuwahamasisha wafanyakazi wa jeshi la nchi hiyo kuhifadhi Qur'ani Tukufu, kutambua suna za Mtume (saw) na kueneza thamani za kusameheana, mazungumzo na mshikamano kati ya matabaka mbalimbali ya jamii.
Sherehe za ufunguzi wa masomo hao zimehudhuriwa na viongozi wa ngazi na taasisi mbalimbali akiwemo Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Yemen Hamoud Abdul Hamid. 681189
captcha