Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa Russia Yulia Latinina amewatuhumu Waislamu kuwa ni watu wanaopenda ghasia na machafuko na wanaounga mkono ugaidi, suala ambalo limepingwa vikali na Waislamu wa Russia.
Katika uchambuzi wake wa kila wiki kupitia Redio Echo ya Moscow, Latinina amedai kuwa Waislamu wa Misri na nchi nyingine za Kiislamu walifurahia milipuko ya mabomu iliyotokea Pakistan na kujeruhi mamia ya watu wasiokuwa na hatia yoyote.
Mchambuzi huyo mwenye misimamo mikali wa Russia amekituhumu Chuo cha al Azhar cha Misri kuwa kinatayarisha magaidi.
Ameongeza kuwa Waislamu wanafurahishwa na vitendo vya kigaidi na kwamba vyuo vikuu katika ulimwengu wa Kiislamu vinalea na kutayarisha magaidi.
Matamshi hayo yasiyokuwa ya kuwajibika ya mchambuzi huyo mwenye misimami ya kufurutu mipaka wa Russia yametolewa katika hali ambayo Russia inatambuliwa kama mwanachama mtazamaji katika Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC na ina uhusiani mkubwa na nchi za Kiislamu. 686704