Sayyid al Qubanchi ambaye alikuwa akihutubia katika swala ya Ijumaa ya jana alitoa mkono wa pole kwa familia za makumi ya raia wa Kikristo wa Iraq waliouawa wakifanya ibada katika kanisa hilo.
Hatibu wa swala ya Ijumaa ya Nafaf ameitaka pia serikali ya Iraq kuimarisha ulinzi wa Wakristo na Wairaqi wote kwa ujumla. Amesema kuwa mauaji ya kanisa la Our Lady of Salvation ni maafa ya kibinadamu ambayo yamedhihirisha udhaifu wa vyombo vya usalama vya Iraq katika shughuli za kuokoa watu waliokuwa wametekwa nyara.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Sayyid Sadruddin Qubanchi amezungumzia siku ya kuuawa shahidi Imam Muhammad Taq (as) inayosadifiana na tarehe 30 Dhil Qaada na akasema kuwa kutambua maarifa na fiqhi ya Ahlul Bait ndio sababu ya kuboresha maisha yetu.
Vilevile amewataka mahujaji waliokwenda Makka kutekeleza ibada ya hija kuoyesha umoja na mshikamano na kujikurubisha zaidi kwa Mola Karima. 689239