IQNA

Paris, mwenyeji wa kikao cha "Uhuru wa Dini na Suala la Jamii za Waliowachache Mashariki ya Kati"

11:02 - November 20, 2010
Habari ID: 2034122
Kikao cha "Uhuru wa Dini na Suala la Jamii za Waliowachache katika eneo la Mashariki ya Kati" kitafanyika tarehe 22 Novemba katika Taasisi ya Utamaduni wa Kiislamu mjini Paris, Ufaransa.
Kikao hicho kitahudhuriwa na wanasiasa, wataalamu wa masuala ya utamaduni na jamii na viongozi wa kidini wa Kiislamu na Kikristo.
Sabah Mahmoud, mtaalamu wa anthropolojia katika Chuo Kikuu cha California atahutubia kikao hicho akiwasilisha uchunguzi wake wa miaka kadhaa kuhusu uhuru wa dini na utamaduni katika eneo la Mashariki ya Kati na Ulaya.
Vilevile Philipe Natwin ambaye pia ni mtaalamu wa anthropolojia anayefanya uchunguzi kuhusu ibada za Waislamu katika eneo la Goutte d' Or mjini Paris na msikiti wa al Fat'h, atazungumzia uhuru wa kidini wa Waislamu na utekelezaji wa ibada za kila siku katika misikiti ya Paris. 697795

captcha