Akizungmza na IQNA, Ustadh Shazli ambaye atakuwa jaji katika Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qurani kwa Ajili ya Wanachuo Waislamu amesema mazingira mazuri ya Qurani nchini Iran yanawahimiza vijana kujifunza na kuhifadhi Qurani.
“Mwanazuoni wa Qurani nchini Iran Abdul Rasul Abayi aliwahi kuniambia kuwa kati ya yanayopewa kipaumbele na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kueneza thamani za Qurani na kwa kweli jambo hili linapaswa kupongezwa”.
Kuhusu Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qurani kwa Ajili ya Wanachuo Waislamu yatakayofanyika mwezi ujaon nchini Iran, Ustadh Shazli amesema mashindano hayo ni ishara ya wazi ya juhudi za Iran zenye lengo la kueneza utamaduni wa Qurani Tukufu miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Amesema mashindano ya Qurani hufanyika katika nchi kama Misri, Malaysia, Bahrain, Qatar, Tunisia, Libya, Morocco, Saudi Arabia n.k, hatahivyo mashindano ya Qurani kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika ulimwengu wa Kiislamu ni hatua isiyo ya kawaida.
Ustadh Farajullah Shazli ni Naibu Mkuu wa Jumuiya ya Maqari na Mahafidh wa Qurani Misri. Aidha ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Al Azhar.
Mashindano ya Tatu ya Kimataifa ya Qurani kwa Ajili ya Wanachuo Waislamu yanatazamiwa kufanyika Januari 9-11 katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran.
703130