IQNA

15:21 - December 05, 2010
Habari ID: 2042141

ISESCO yatoa wito wa kuwepo umoja wa umma wa Kiislamu

Katibu Mkuu wa Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO Dr Abdulaziz Othman al Tuwaijri ametoa ujumbe kwa mnasaba wa kukaribia mwaka mpya wa Hijria Qamariya na kuwataka Waislamu duniani kote wawe na umoja na mshikamano zaidi ili waweze kukabiliana na vitisho vya maadui.

Kwa mujibu wa tovuti ya ISESCO al Tawaijri ametoa ujumbe ambapo ameashiria umuhimu wa umoja wa Umma wa Kiislamu na kutoa wito wa kujiweka mbali na aina yoyote ya unafiki wa kisiasa na kimadhehebu. Amesema umoja wa Waislamu utauwezesha umma wa Kiislamu kukabiliana ipasavyo na vitisho vilivyopo.
Katibu Mkuu wa ISESCO amesema kuna ulazima wa kuimarisha udugu wa Kiislamu na kuongeza kuwa: "Waislamu duniani wanapaswa kushirikiana zaidi katika nyanja mbalimbali hasa za kiuchumi ili kuziwezesha nchi za Kiislamu kupiga hatua zaidi za maendeleo. 706024

captcha