Mkuu wa mkoa wa Karbala Aamaluddin al Harr amesema kuwa ofisi yake imetayarisha suhula zinazohitajika kwa ajili ya kukaribisha na kuwahudumia wafanyaziara katika mji huo mtakatifu kwenye siku ya Ashura, yaani tarehe kumi Muharram.
Ameongeza kuwa mkoa wa karbala unahitaji bajeti zaidi kwa ajili ya kutayarisha huduma na suhula bora zaidi kwa wafanyaziara wa Imam Hussein na ndugu yake Abbas (as) wanaokwenda mjini humo wakati wote hususan katika minasaba ya kidini.
Aamaluddin ameongeza kuwa takwimu rasmi kuhusu idadi ya wafanyaziara waliokwenda mjini humo kwa ajili ya ziara ya siku ya Ashura mwaka jana ilikuwa milioni tatu na maelfu miongoni mwao walitokea nchi za Ghuba ya Uajemi, Pakistan, Iran, Uturuki, Lebanon na baadhi ya nchi za Ulaya.
Wafanya ziara milioni thalathini huenda Karbala kila mwaka kwa ajili ya kuzuru kaburi la mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein (as). 709246