Kongamano hilo linadhaminiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Nchi za Kiislamu ISESCO. Shirika hilo linashirikiana na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa pamoja na Kamisheni ya Kitaifa ya Elimu, Sayansi na Utamaduni ya Sudan katika kuandaa kongamano hilo.
Zaidi ya wasomi na wanafikra kutoka nchi kadhaa za Kiislamu watashiriki katika kongamano hilo kwa ajili ya kuchunguza njia za kushajiisha uwekezaji katika sekta ya elimu ya watu wazima katika nchi za Kiislamu, wanachama wa Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC.
Kuimarishwa nguvu kazi, usimamiaji fedha na mifumo ya kifedha pamoja na kuimarisha mawasiliano ya taasisi zinazohusika na uwekezaji katika sekta iliyotajwa ni baadhi ya mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo. 717629