IQNA

12:32 - January 04, 2011
Habari ID: 2058302

Mtanzania aliyesilimu Yemen atunukiwa zawadi za Qur'ani

Raia mmoja wa Tanzania huko Yemen ametaja Shahadatein (Shahada Mbili) mbele ya Kamati ya Waqfu ya Muongozo wa Kiislamu katika mkoa wa Aden na kuikubali dini ya Kiislamu. Muislamu huo mpya amepewa zawadi Qur'ani Tukufu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA tawi la Tanzania, Mkurugenzi wa Kamati ya Waqfu ya Muongozo wa Kiislamu katika mkoa wa Aden amesema kuwa,' Alfrim Yohana, raia wa Tanzania mwenye umri wamiaka 33 ambaye kwa muda sasa amekuwa akijifunza Uislamu na Qur'ani Tukufu, baada ya utafiti wake na kuufahamu Uislamu kikamilifu, ameamua kusilimu.
Baada ya kuukubali Uislamu Yohana amebadilisha jina lake na kupewa jina la Abdulazizi na hivi sasa anaendeleza utafiti wake kuhusu Uislamu ili kuufahamu zaidi.
Punde baada ya kusilimu Wizara ya Waqfu na Muongozo wa Kiislamu Yemen imemkabidhi Qur'ani Tukufu iliyotarjumiwa kwa lugha ya Kiswahili. 607349

captcha