IQNA

Ushirikiano wa Mashia na Masuni wa Saudia katika kukabiliana na misimamo mikali

14:24 - January 15, 2011
Habari ID: 2064745
Mwanaharakati wa sheria wa Saudi Arabia Issa al Ghaith ambaye pia ni jaji wa Wizara ya Sheria ya nchi hiyo ametoa wito wa kuwepo ushirikiano na mshikamano kati ya maulama wenye misimamo ya wastani wa Kishia na Kisuni kwa ajili ya kukabiliana na makundi yenye misimamo mikali na ya kuchupa mipaka.
Issa al Ghaith amesema hitilafu zote za kimadhehebu katika historia zinarejea kwenye matakwa ya kidunia yanayopakwa rangi ya dini, na maulama wa Kiislamu wanaweza kubadili hitilafu hizo na kuanzisha ushirikiano badala yake.
Mwanaharakati huyo wa Saudi Arabia amesisitiza katika kikao hicho kilichohudhuriwa na shakhsia, waandishi, wanafikra na wanazuoni wa kidini wa miji ya Qatif na Dammam juu ya udharura wa kuwepo umoja na mshikamano katika kipindi nyeti cha sasa.
Sheikh Hassan Saffar mwanazuoni wa Kiislamu wa Kishia wa Saudi Arabia ambaye pia alihudhuria kikao hicho amesema kuwa maadui wa Kiislamu wamekuwa wakifanya njama za kuanzisha hitilafu na migawanyiko katika umma wa Kiislamu na kwamba ni wajibu wa maulama kulinda umoja na mshikamano wa Kiislamu.
Sheikh Hassan Saffar amesisitiza juu ya mshikamano wa Waislamu wa madhehebu ya Shia na Suni nchini Saudi Arabia na kusema kuwa umoja na mshikamano ni thamani ya Kiislamu na wala si wenzo wa kufikia malengo ya kimakundi na kibinafsi. 730527

captcha