IQNA

16:10 - January 17, 2011
Habari ID: 2066154

Mkutano wa kimataifa wa kutetea Quds na Palestina wafanyika Istanbul

Mkutano wa kimataifa wa kutetea Quds na Palestina umefanyika mjini Istanbul Uturuki ambapo shakhsia kutoka nchi 50 tofauti za Kiislamu na Kiarabu walihudhuria.

Kwa mujibu wa tovuti ya Palestine info mkutano huo ulichunguza na kujadili njia za kuunga mkono na kutetea Quds Tukufu na jinsi ya kuleta uthabiti na utulivu katika ardhi za Palestina. Hati ya kuunga mkono Quds na Palestina pia iliratibiwa na kuchapishwa na mkutano huo. Hati hiyo inasisitiza kwamba Palestina ni ardhi ya Kiarabu na Kiislamu ambayo inamilikiwa na Wapalestina peke yao na kwamba utawala ghasibu wa Israel ni utawal usio halali unaozikalia ardhi hizo kwa mabavu.
Hati hiyo inasisitiza haki ya kurejea wakimbizi wote wa Kipalestina katika ardhi zao za jadi ambazo zinakaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel. Inasema kuwa hatua ya uchokozi na dharau ya utawala huo katika maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo na hasa Msikiti wa al-Aqsa ni tishio kubwa kwa usalama na amani ya Mashariki ya Kati.
Katika taarifa hiyo, udharura wa kufanyika juhudi maradufu za kuunga mkono taifa la Palestina na kutatuliwa suala la Palestina na nchi za Kiislamu na Kiarabu ni jambo jingine ambalo limetiliwa mkazo. Washiriki wa mkutano huo wametangaza kwamba wakiwa wawakilishi wa jumuiya za kiraia wako tayari kushirikiana kikamilifu na pande zote husika kwa ajili ya kuwasaidia Wapalestina na kutekeleza miradi ya pamoja ya kimataifa kwa shabaha ya kutetea Quds na Palestina. 731214
captcha