Huku wakiashiria upinzani wa wazi wa Zainul Abidin dhidi ya mafundisho ya dini, wanazuoni hao wamesema kuwa inajuzu kisheria kuangushwa kwa serikali hiyo.
Abdul Mu'ata Biyumi, mwanachama wa jopo la uhakiki wa Kiislamu la al-Azhar amesema kuhusiana na suala hilo kwamba wananchi wanawajibika kukabiliana na mtawala yoyote yule ambaye hatekelezi ahadi zake, kupinga wazi mafundisho na sheria za Mwenyezi Mungu na kueneza ufisadi katika jamii.
Muhammad Raf'at Othman mwanachama mwingine wa jopo hilo amesema kwamba kuangushwa kwa utawala wa Zainul Abidin bin Ali kunajuzu kutokana na kuwa askari usalama wa utawala huo walikabiliana kwa nguvu ya ziada na waandamanaji na kuwakandamiza watu waliokuwa wakiandamana kwa amani kwa ajili ya kufuatilia matakwa yao halali.
Dikteta Zainul Abidin bin Ali ambaye kwa muda wa miaka 23 ametawala Tunisia kwa mabavu na kupinga vikali sheria na mafundisho ya Kiislamu, aling'olewa madarakani hivi karibuni na wananchi wa nchi hiyo. 733011