Tovuti ya Islam Today imeripoti kuwa kwa mujibu wa sheria hiyo mpya wanawake wa Kiislamu wa Argentina wanaweza kutumia picha waalizopiga wakiwa na vazi la hijabu katika vitambulisho vyao.
Sheria hjiyo mpya imepasishwa kutokana na juhudi za Rais Cristina Fernandes wa Argentina za kustawisha uhuru wa dini na uhuru wa kujieleza.
Rais Fernandes amesema ujumbe wa serikali ya Argentina kwa nchi mbalimbali duniani ni kuwa tofauti zinaweza kufumbiwa macho kwa shabaha ya kufikia malengo ya juu zaidi na wala si sawa kutwishana mitazamo mbalimbali hususan katika uwanja wa masuala ya kidini.
Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa mwaka 2009 na kituo cha Pew Research Center, Waislamu wanaunda asilimia mbili ya jamii ya Argentina. 738278