IQNA

Tafsiri ya al Kashif ya Allamah Mughniya imeathiriwa na masuala ya kisiasa na kijamii

15:02 - January 30, 2011
Habari ID: 2072559
Marehemu Allamah Muhammad Jawad Mughniya aliathiriwa na masuala ya kisiasa na kijamii ya wakati huo katika tafsiri yake ya al Kashif.
Katika kusherehesha aya za Qur'ani, msomi huyo wa Kiislamu alijadili masuala kama njama za Israel za kutaka kupotosha Uislamu na Qur'ani kwa kadiri kwamba maudhui hiyo ya kufichua njama za Banii Israel inaunda kitabu kikubwa.
Hapana shaka kwamba wafasiri wengi wa Qur'ani wameathiriwa na mazingira, masuala na maswali yaliyokuwa yakiulizwa zaidi katika zama zao kama inavyoshuhudiwa katika tafsiri za wasomi wakubwa wa Kiislamu kama al Tafsrul Kabiir ya Fakhru Razi, al Jawahir ya Tantawi na vilevile al Kashif ya Allamah Mughniya. Mwanazuoni huyo mkubwa wa Kiislamu alijadili masuala mengi ya kisiasa na kijamii, jinai za Israel na njama za Banii Israel za kutaka kupotosha Qur'ani na Uislamu katika tafsiri yake. Kwa mfano tu amezungumzia kadhia ya mauaji yaliyofanywa na Wayahudi dhidi ya watoto wadogo na watu wasojiweza katika vita vya mwaka 1967 na kufichua malengo lya Israel na waitifaki wake. Allamah Muhammad Jawad Mughniya anasema katika tafsir ya al Kashif kwamba operesheni za kujitolea kufa shahidi kwa ajili ya kulinda nchi ni bora zaidi kuliko kuishi maisha duni na ya kudhalilishwa.
Tafsri ya al Kashif ni moja ya athari bora zaidi za Allamah Muhammad Jawad Mughniya na ameiandika kwa kutumia mbinu ya tartibi kwa maana ya kufasiri aya za Qur'ani moja baada ya nyingine kuanzia mwanzo hadi mwisho wa sura za Qur'ani Tukufu. Tafsiri hiyo iliandikwa katika kipindi cha vita vya ndani vya Lebanon na wakati wa vita vya Waarabu na Israel. Kwa mujibu mfasiri huyo mwenyewe sehemu ya mwisho ya juzuu ya sita ya tafsiri ya al Kashif ilikamilishwa mwaka 1390 Hijria katika mji mtakatifu wa Kabala.
Tafsiri ya al Kashif ni miongoni mwa vitabu vya mwisho vya Allamah Mughniya na mfasiri huyo anaamini kwamba fikra zake na mbinu yake ya uandishi imedhihiri zaidi katika kitabu hicho. 738117

captcha