IQNA

Maimamu wa misikiti wataka kuanzishwa shule kamili ya Kiislamu Carolina

13:22 - January 31, 2011
Habari ID: 2073096
Maimamu wa misikiti katika mji wa Winstone- Salem katika jimbo la Carolina Kaskazini nchini Marekani wametaka kuasisiwa kwa shule kamili na ya nyakati zote ya Kiislamu katika mji huo katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Kwa mujibu wa tovuti ya Journalnow, Imam Khalid Grings wa moja ya misikiti ya Winston-Salem amesema kuwa yeye na Waislamu wenzake wa mji huo wamekuwa wakifuatilia kwa karibu malengo ya kuanzishwa shule hiyo binafsi katika mji huo katika muda wa miaka miwili ijayo.
Imam Khalid Grings amesema tayari shule kama hizo zimeanzishwa katika miji mingine mingi ya jimbo hilo.
Amesema licha ya kuwa kuna shule kadhaa zinazofundisha masuala ya Kiislamu katika mji huo lakini shule hizo hazifai na wala hazitoi masomo ya kutosha kwa wanafunzi wa Kiislamu.
Kwa mujibu wa takwimu za Marekani za mwaka 2008 kuna shule 235 za Kiislamu za watu binafsi nchini humo. Shule hizo zote ni za msingi. 738883
captcha