IQNA

Muungano wa Kimataifa wa Maulamaa walaani ukandamiza wa wananchi Libya

22:29 - February 22, 2011
Habari ID: 2084974
Muungano wa Kimataifa wa Maulamaa wa Kiislamu umetoa taarifa ukilaani ukandamizaji na mauaji yanayofanywa na serikali ya Libya dhidi ya wananchi wanaoandamana kupinga utawala wa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi.
Taarifa ya muungano huo imeitahadharisha serikali ya Libya juu ya kuendelezwa umwagaji damu. Imeutaka utawala wa Libya kumcha Mungu katika kuamiliana na wananchi uliowatawala kwa zaidi ya miongo minne na kuogopa adhamu ya Mwenyezi Mungu. Imesema serikali ya Libya inapaswa kuwapa wananchi haki yao ya kujiamulia hatima yao na kufanya marekebisho ya kimsingi.
Vilevile taarifa ya Muungano wa Kimataifa wa Maulamaa wa Kiislamu imeitahadharisha serikali ya Libya kuhusu utumiaji wa silaha za kisasa dhidi ya wananchi.
Taarifa hiyo pia imewataka wanajeshi wa Libya kuacha kukabiliana na wananchi. Aidha imewahimiza wananchi kusimama kidete katika kudai haki zao. 751816
captcha