IQNA

Mfalme wa Bahrain aamuru kuachiwa huru wanaharakati wa Kishia

15:34 - February 23, 2011
Habari ID: 2085503
Mfalme wa Bahrain ameamuru kuachiwa huru wanaharakati wanaoshikiliwa katika jela za nchi hiyo na kusimamishwa kesi zao mahakamani kufuatia maandamano makubwa yanayofanywa na maelfu ya wananchi dhidi ya utawala wa nchi hiyo.
Mfalme Sheikh Hamad bin Issa Al Khalifa wa Bahrain ameamuru kuachiwa huru wanaharakati waliko jela na kusimamishwa kesi zao.
Kwa upande mwingine mwakilishi wa chama cha al Wifaq cha Mashia waliowengi nchini Bahrain Abdul Jalil Ibrahim ambaye pia ni miongoni mwa wapinzani wa utawala wa nchi hiyo amesema inatazamiwa kuwa wanaharakati 25 wa kambi ya upinzani wataachiwa huru.
Ameongeza kuwa kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa ni moja kati ya matakwa ya wapinzani wanaoandamana kwa ajili ya kukubali kufanya mazungumzo na serikali ya Bahrain. 752493

captcha