IQNA

Erdogan: Propaganda chafu za kuwatisha watu kuhusu Uislamu ni jinai dhidi ya binadamu

23:43 - March 01, 2011
Habari ID: 2088835
Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyep Erdegan amesema propaganda chafu za kuwatisha watu kuhusu Uislamu ni jinai dhidi ya binadamu.
Gazeti la al Hayat linalochapishwa nchini Saudi Arabia limemnukuu Erdogan akiwahutubu wahajiri wa Kituruki katika mji mmoja nchini Ujerumani kwamba Ankara ina wasiwasi mkubwa kuhusu mwenendo wa kuuchafulia jina Uislamu katika baadhi ya nchi za Ulaya hususan Ujerumani na inawataka wanasiasa na vyombo vya habari kuacha kuchochea mwenendo huo.
Waziri Mkuu wa Uturuki ameongeza kuwa kuwatisha watu kuhusu Uislamu ni jinai dhidi ya binadamu kama ambavyo kufanya uadui dhidi ya dini ni kosa la jinai.
Recep Tayyep Erdogan amewataka pia Waturuki wanaoishi Ujerumani kujiunga na jamii ya nchi hiyo na wakati huo huo walinde utamaduni wao. 755909
captcha