IQNA

Vituo vya intaneti vinavyovunjia heshima Uislamu vyafungwa Pakistan

20:17 - March 02, 2011
Habari ID: 2089485
Serikali ya Pakistan imechukua hatua ya kufunga vituo vya intaneti vinavyopiga vita Uislamu baada ya vituo kadhaa kukivunjia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani na Mtume Muhammad (saw).
Gazeti la Times of India limemnukuu Naibu Naibu Mwanasheria Mkuu wa Pakistan Naveed Inayat Malik akisema kuwa Jumuiya ya Mawasiliano na Wizara ya Teknolojia ya Pakistan zimechukua hatua ya kufunga vituo vyote vya intaneti vinavyovunjia heshima matukufu ya Kiislamu.
Ameongeza kuwa serikali imeunda kamati maalumu ya kusimamia vituo vya intaneti.
Mkuu wa Mahakama Kuu ya Pakistan Ijaz Choudary amesema kamati hiyo ya serikali inawajibika kutoa ripoti kwa Mahakama Kuu kuhusu shughuli na kazi zake. 756618

captcha