Hayo yamesemwa na Sheikh Ahmad al Qattan ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa wa Kisuni wa Lebanon na Mwenyekiti wa jumuiya ya "Qauluna Wal-amal." Amesema katika harakati ya sasa ya wananchi, Waislamu wanatangaza kuwa hawawezi tena kunyamaza kimya na umewadia wakati wa kutupilia mbali vibaraka na madikteta ili umoja wa Kiislamu uweze kupatikana.
Sheikh Ahmad al Qattan amesema kuwa Waislamu wanapaswa kutilia maanani maslahi ya Uislamu na kuyaona kuwa ndio msingi wa maamuzi yao ili kuimarisha umoja na mshikamano.
Amesema Uislamu ni mpana mno na unaweza kukusanya pamoja Waislamu wa mirengo na makundi yote ingawa baadhi ya Waislamu wameamua kubana duara hilo kubwa na kudhoofisha safu za Waislamu.
Mwanafikra huyo wa Lebanon amesisitiza kuwa ili kuweza kufikia umoja wa Kiislamu tunapaswa kuambatanisha nadharia na vitendo na tunaweza kusimama kidete kwa pamoja dhidi ya maadui chini ya kivuli cha Uislamu unaokutanisha wafuasi wote wa dini hiyo tukufu na kuwafukuza wakoloni. 756991