Akiashiria harakati za wananchi na hasa katika nchi za Misri na Libya, Ayatullah Muhammad Emami Kashani ameeleza kusikitishwa kwake na mauaji yanayofanywa dhidi ya wananchi wa Libya na kusisitiza kuwa, kuhuishwa harakati za wananchi ni sawa na kuhuishwa thamani za Kiislamu. Ayatullah Kashani amesema, kama wananchi wa eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu wa Kiislamu wanataka harakati zao zifikie malengo yanayokusudiwa, wanapaswa kuhuisha fikra za kumsubiri Imam Mahdi AS. Khatibu wa sala ya Ijumaa amesema kuwa, moja kati ya sababu kuu za kupatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa uongozi wa Imam Khomeini MA, ni kuhuishwa fikra ya kumsubiri Imam wa Zama. Amesisitiza kuwa, Iran imepiga hatua kubwa kimaendeleo na kwamba leo hii wananchi wa Iran wamesonga mbele katika nyanja zote. Ayatullah Kashani amenukuu matamshi yaliyotolewa jana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kigezo kizuri kwa wananchi wa eneo la Mashariki ya Kati na ulimwengu wa Kiislamu.
761584