IQNA

14:06 - March 19, 2011
Habari ID: 2097493

Ayatullah Jannati: Marekani ndiyo mtenda jinai mkubwa zaidi

Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran amesema leo kuwa Marekani ndio mhusika na mtendaji mkuu wa jinai katika eneo la Mashariki ya Kati.

Ayatullah Ahmad Jannati amesema kuwa Marekani imeonesha wazi sura ya bundi katika kukabiliana na serikali zinazowakandamiza wananchi katika eneo hili.
Akifafanua zaidi Ayatullah Jannati amesema kwa upande mmoja Marekani imekuwa ikitoa maneno makali dhidi ya serikali ambazo haziungi mkono ajenda za Washington na kuzitaka zisikize sauti za wananchi wanaoandamana na kwa upande wa pili imekuwa ikinyamazia kimya jinai dhidi ya wananchi zinazofanywa na madikteta ambao ni vibaraka wa Washington.
Akitoa mifano ya Saudi Arabia na Bahrain, Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran amesema kwa kuzingatia ukweli kwamba viongozi wa nchi hizo ni watumwa wa Marekani, Watawala wa Washington wamechelea kukosoa hatua zao za kuwakandamiza wananchi ilhali katika nchi zingine kama Libya, Marekani imesonga mbele na kuhakikisha maazimio yanapitishwa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani mauaji na udhalilishwaji wa wananchi.
765504
captcha