IQNA

10:40 - April 05, 2011
Habari ID: 2100642

Mkurugenzi Mkuu wa ISESCO kushiriki katika kikao cha kimataifa cha mazungumzo ya tamaduni

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO Dr. Abdulazizi Othman Altwaijri atashiriki katika Kikao cha Kimataifa ya Mazungmumzo Baina ya Tamaduni kitakachofanyika Baku, mji mkuu wa Jamhuri ya Azerbaijan kati ya Aprili 7-9.

Katika kikao hiki ambacho kimeandaliwa na Wizara ya Utamaduni ya serikali ya Azerbaijan, Mkurugenzi wa ISESCO atahutubia kikao hicho. Hotuba yake itahusu utandawazi na athari zake katika uhusiano wa kiutamaduni.
768784
captcha