IQNA

16:35 - April 11, 2011
Habari ID: 2104198

Onyo la mwanazuoni wa Iraq dhidi ya kuharibiwa makaburi ya viongozi wa Kishia nchini Misri

Sheikh Khalid al-Mulla, Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Kisunni wa Kusini mwa Iraq ametoa taarifa akionya dhidi ya kutokea fitina za kimadhehebu katika ulimwengu wa Kiislamu kutokana na baadhi ya makundi yaliyo na misimamo ya kupindukia mipaka kuchochea vitendo vya kuharibu makaburi ya viongozi wa Kishia pamoja na maeneo yao ya ibada nchini Misri.

Sheikh al-Mulla amesema katika taarifa yake kwamba tayari uchochezi wa makundi hayo umepelekea kuchomwa moto makaburi ya viongozi wa Kishia katika baadhi ya mikoa ya Misri jambo ambalo limeamsha hasira ya watu wa Misri na kupelekea wanazuoni wa al-Azhar pamoja na Mufti wa Misri kulaani vikali kitendo hicho kisicho cha kiutu. Amewasifu wanaozuoni hao wa Misri kutokana na msimamo wao wa kukemea kuharibiwa na kuchomwa moto makaburi ya mawalii wa Mwenyezi Mungu wa madhehebu ya Shia na kuongeza kuwa lengo la wahusika wa kitendo hicho cha aibu ni kuzusha fitina na mfarakano katika ulimwengu wa Kiislamu. Sheikh al-Mulla amewataka wanazuoni wote wa Kiislamu kuchukua hatua za dharura ili kuzuia kukaririwa kwa vitendo kama hivyo vya uchochezi wa kimadhehebu. 771541
captcha