IQNA

12:01 - April 19, 2011
Habari ID: 2108304

Wanazuoni wa Lebanon walaani hatua ya kubomolewa Misikiti nchini Bahrain

Jumuya ya Maulama wa Jabal Amil ya nchini Lebanon imetoa taarifa ikilaani vikali hatua ya watawala wa Bahrain wakishirikiana na wa Saudi Arabia ya kubomoa misikiti ya Waislamu nchini humo.

Katika taarifa yao, maulama hao wamesema kuwa ubomoaji wa misikiti nchini Bahrain ni ishara ya wazi ya kufanyika uchochezi dhidi ya Waislamu na kuwataka wanazuoni na mashirika ya Kiislamu katika nchi zote kulaani vikali kitendo hicho. Maulama hao pia wamelaani hatua ya watawala wa Bahrain ya kuwafukuza nchini humo raia wa Lebanon kwa visingizio visivyo na msingi na kusisitiza kuwa hilo ni jambo lisilohalalishwa wala kukubalika kwa njia yoyote ile. 776340
captcha