IQNA

11:13 - April 20, 2011
Habari ID: 2108944

Mwanajeshi wa Uingereza aliyekosea heshima Qur'ani afungwa jela siku 70

Mahakama moja ya Uingereza siku ya Jumatatu ilimfunga jela kwa siku 70 mwajeshi mmoja wa zamani wa nchi hiyo kwa shtaka la kukosea heshima Qur'ani Tukufu.

Mwanajeshi huyo wa zamani kwa jina la Andrew Ryan mwenye umri wa miaka 32 amefungwa jela kutoka na kosa la kuiba Qur'ani Tukufu katika mkataba moja ya mji wa Carlisle nchini Uingereza na kuzusha vurugu la kidini miongoni mwa wenzake. Baada ya kuiba Qur'ani kwenye maktaba hiyo hapo tarehe 19 Januari 2011, mwanajeshi huyo asiye na aibu aliichoma moto hadharani mbele ya wanunuzi na wanafunzi wa shule. Akitoa hukumu dhidi ya Ryan jaji aliyeendesha kesi yake alisema kuwa kitendo hicho cha chuki kiliendeshwa kwa mpangilio maalumu na kwamba aliichomo moto Qur'ani kwa makusudi ya kueneza propaganda dhidi ya kitabu hicho kitakatifu. Hukumu hiyo imetolewa dhidi ya Ryan wiki moja baada ya kutiwa mbaroni mwanachama mmoja wa Chama cha Taifa cha Uingereza kwa kosa la kuchoma moto Qur'ani kwenye uwanja wa nyumba yake. 776963
captcha