IQNA

16:41 - April 30, 2011
Habari ID: 2114596

Maandamano ya Mashia wa Saudi Arabia ya kufungamana na watu wa Bahrain

Mashia wa Saudi Arabia wanoishi katika eneo la as-Sharqiyya jana Ijumaa walifanya maandamano makubwa ya kuungana na Waislamu wenzao wa Bahrain wanaokandamizwa na watawala dhalimu wa nchi hiyo.

Wakazi wa mji wa Awamiya walijitokeza kwa wingi katika maandamano hayo na kupiga nara za kuunga mkono na kufungamana na Waislamu wenzao wa Bahrain mara tu baada ya kumalizika swala ya Ijumaa.
Waandamanaji hao walitaka kuondolewa kwa askari jeshi wa Saudi Arabia waliopelekwa Bahrain kwa ajili ya kushirikiana na jeshi la nchi hiyo kuwakandamiza waandamanaji wanaopigania haki zao kutoka kwa watawala wa uko wa Aal Khalifa wanaotumia mbinu zote za kinyama kuwakandamiza waandamanaji. Waandamanaji wa Awamiya pia walitaka kuachiliwa huru wafungwa wote wa kisiasa wanaoshikiliwa katika jela za utawala wa Saudi Arabia.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Waislamu wa Kishia wa Saudi Arabia wamekuwa wakifanya maandamano ya kulalamikia ukandamizaji unaofanywa na utawala wa nchi hiyo na vilevile wa Bahrain dhidi ya Mashia wa nchi hizo. 783396
captcha