IQNA

Saudi Arabia yazidisha udhibiti wa vyombo vya habari

13:01 - May 01, 2011
Habari ID: 2115183
Serikali ya Saudi Arabia imezidisha udhibiti na usimamizi juu ya utendaji wa vyombo vya habari nchini humo kwa kisingizio cha eti kukabiliana na uenezaji wa mambo yanayokwenda kinyume cha sheria za Kiislamu.
Hata hivyo wakosoaji wanasema hatua hiyo imechukuliwa kwa lengo la kuchuja habari zinazohusiana na mauaji yanayofanywa dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Bahrain.
Wiki hii serikali ya Riyadh iliwatia nguvuni waandishi wawili wa weblogu wafuasi wa madhehebu ya Shia kwa kile kilichotajwa ni kuvuruga usalama wa taifa.
Sheria mpya ya vyombo vya habari imeanza kutekelezwa huku mkaguzi wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia akitangaza kuwa zaidi ya watu 160 ambao wengi wao ni wafuasi wa madhehebu ya Shia wametiwa nguvuni nchini humo kwa tuhuma ya kuchapisha habari katika weblogu zao.
Harakati ya mapambano na wimbi kubwa la mwamko wa Kiislamu linaloshuhudiwa katika nchi jirani na Saudi Arabia zimewatia kiwewe viongozi wa Riyadh na hapana shaka kuwa kupasishwa kwa sheria mpya ya vyombo vya habari kunafanyika kwa lengo la kuzuia upashaji habari unaohusiana na mapambano ya wananchi dhidi ya tawala za kidikteta kama ule wa Bahrain unaoendelea kutekeleza mauaji dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia. 784179
captcha