Taarifa ya shirika hilo imesema hukumu iliyotolewa na mahakama ya kijeshi dhidi ya watu hao waliotiwa nguvuni katika maandamano ya kulalamikia ukandamizaji wa utawala huo dhidi ya watu wasio na hatia inapaswa kufutwa mara moja.
Shirika hilo pia limetaka waandamanaji wengine waliotiwa nguvuni na utawala wa Bahrain bila kuruhusiwa kuonana na mawakili wao waachiliwe huru mara moja.
Joe Stork, naibu mkuu wa shirika hilo katika kanda ya Mashriki ya Kati na Afrika Kaskazini amesema kuwa hakuna uwezekano wowote wa mahakama hiyo ya kijeshi kuendesha mashtaka dhidi ya watuhumiwa kwa audilifu na kwa mujibu wa sheria, likiwemo suala la kuwaruhusu wawakilishwe na mawakili wao.
Watu saba waliofikishwa mbele ya mahakama hiyo ya kijeshi ni raia wa kwanza wasiokuwa wanajeshi kuwahi kuhukumiwa katika mahakama hiyo ya kuogofya. 785682