IQNA

Imarati mwenyeji wa kikao cha 'Nafasi ya Wakfu katika Harakati ya Kielimu ya Kiislamu'

13:02 - May 05, 2011
Habari ID: 2117756
Chuo cha Masuala ya Kidini na Utafiti wa Kiislamu kinachofungamana na Chuo Kikuu cha Sharja katika Umoja wa Falame za Kiarabu kimeandaa kikao cha 'Nafasi ya Wakfu katika Harakati ya Kielimu ya Kiislamu' ambacho kimepangwa kufanyika tarehe 19 baadaye mwezi huu.
Kwa mujibu wa gazeti la Imarati la al-Khalij, hicho kitakuwa kikao cha kumi kuandaliwa na chuo kilichotajwa ambapo wasomi na wanafikra kutoka nchi mbalimbali hushiriki na kutoa maoni yake kuhusiana na masuala tofauti ya Kiislamu.
Waandaaji wa kikao hicho wamesema kuwa wamechagua mada ya wakfu kujadiliwa katika kikao cha mwaka huu kutokana na nafasi muhimu ya wakfu katika kunyanyua uchumi wa ulimwengu wa Kiislamu na kuhuisha mfungamano pamoja na udugu wa Kiislamu.
Vyuo 29 kutoka nchi 16 za Kiarabu na Kiislamu na vilevile Marekani pamoja na taasisi kadhaa za utafiti zimealikwa kushiriki katika kikao hicho. 786780
captcha