Mahakama hiyo ilimwachilia huru Ernesto Rojas Abbate mwenye umri wa miaka 30 hapo jana Jumatatu kwa hoja kuwa hakuwa na kesi ya kujibu kuhusiana na tuhuma za dharau na chuki dhidi ya Qur'ani na Waislamu bali ilimkemea tu kutokana na misimamo yake ya kigaidi ambayo ilisema haikuwahusu Waislamu.
Mahakama hiyo imemwachilia huru kijana huyo katika hali ambayo alichoma moto Qur'ani hadharani na kusajili kitendo hicho cha dharau dhidi ya matukufu ya Kiislamu kwenye mkanda wa video na kisha kuusambaza kwenye mtandao wa intaneti mwaka uliopita. 788888