IQNA

22:37 - May 14, 2011
Habari ID: 2121997

Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani kuunda kamati ya uwekezaji

Wanachama wa Baraza la Uendeshaji la Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu wamepasisha uanachama wa jumuiya hiyo katika Muungano wa Jumuiya za Uturuki na kuundwa Kamati ya Ushauri kwa ajili ya uwekezaji.

Uamuzi huo umechukuliwa katika kikao cha 21 cha wanachama wa Baraza la Idara la Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu kilichofanyika jana nchini Saudi Arabia.
Miongoni mwa maudhui kuu zilizojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na kuchunguza matumizi ya Baraza la Idara la Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu katika mwaka 1431 Hijria, suala la kuundwa Baraza la Ushauri la masheikh wa makarii na kupasisha ripoti ya kila mwaka ya Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu. 790811
captcha