IQNA

Kuchapishwa vitabu vya Kiislamu, moja ya njia za kukidhi mahitaji ya jamii ya leo

22:22 - May 22, 2011
Habari ID: 2126520
Nurasima Haj Omar, Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Brunei amesisitiza juu ya udharura wa kutungwa na kuchapishwa vitabu vya Kiislamu kwa ajili ya kukidhi mahitaji tofauti ya jamaii ya sasa.
Kwa mujibu wa tovuti ya Bruneionline akizungumza hapo katika chuo hicho huko Bandar Seri Begawan mji mkuu wa nchi hiyo ya kifalme, Haj Omar amesema kwamba uchapishaji na usambazaji wa vitabu vya Kiislamu utachangia pakubwa katika kunyanyua kiwango cha utamaduni wa Kiislamu katika jamii.
Akizungumza katika sherehe maalumu ya kuzinduliwa kitabu cha Kiislamu cha 'Ijue Elimu ya Hadithi' mhadhiri huyo wa Kiislamu amesema kuwa kuna haja kubwa ya kuzingatiwa na kuungwa mkono juhudi za kuchapishwa na kusambazwa vitabu vya Kiislamu katika jamii kwa sababu kunasaidia sana katika utatuaji wa baadhi ya changamoto zinazoikabili jamii. 796268
captcha