Hayo ni kwa mujibu wa Mohammad Issa, Mkuu wa kitengo cha Huduma za Kibenki za Kiislamu katika Benki ya Stanbic Tanzania.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimatiafa la Kiislamu, INNA, Mohammad Issa amesema kutokana na imani ya dini ya Kiislamu kukataza suala la riba, Waislamu wengi walikuwa hawajajiunga na mfumo wowote wa kibenki kwa kuhofu kupingana na maagizo ya Mtume Mohammad (S.A.W), hivyo hatua ya baadhi ya benki hapa nchini kuanzisha mfumo huo ni ukombozi kwa Waislamu wote.
Amepongeza Benki ya Stanbic kwa kuanzisha huduma za kifedha za Kiislamu ambazo zitatoa huduma kwa idadi kubwa ya Waislamu Tanzania.
Kuanzisha huduma hizo za kifedha za Kiislamu nchini Tanzania ni katika mkondo unashuhudiwa barani Afrika wa ustawi wa mfumo wa kifedha wa Kiislamu.
796354