IQNA

10:20 - June 05, 2011
Habari ID: 2133184

Ahmadinejad: Uistikbari wa leo kikwazo dhidi ya harakati ya tauhidi

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kusisitiza kuwa kambi ya uistikbari imefikia mwisho amesema kwamba hii leo uistikbari ndicho kikwazo dhidi ya kambi ya tauhidi.

Ameongeza kuwa, iwapo kikwazo hicho kitaondolewa basi harakati ya tauhidi itashika kasi na kufikia kwenye ufanisi na mafanikio makubwa. Rais Ahmadinejad amesema hayo usiku wa kuamkia leo katika hafla ya kukumbuka miaka 22 tangu alipofariki dunia Imam Khomeni M.A Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ahmadinejad ameongeza kwamba, taifa la Iran limevunja njama zote za mabeberu kwa uongozi wa busarawa Kiongozi Muadhamu na kusimama kidete taifa la Iran, lakini pamoja na hayo inabidi isisahaulike kuwa mipango na njama hizo bado zinaendelea. Aidha Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameelezea baadhi ya sifa za Imam Khomeini na kusema kwamba, kadiri siku zinavyopita ndivyo Imam Khomeini MA anavyozidi kuwa hai zaidi katika nyoyo za wapenda haki duniani kuliko huko nyuma. Amesema sifa ya kwanza ya Muasisi huyo wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa, maneno na matendo yake yote yalikuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwamba hiyo ndiyo tauhidi ya kweli.
803357
captcha