IQNA

Rais Ahmadinejad: Kuna udharura wa kuarifishwa ugaidi

21:35 - June 07, 2011
Habari ID: 2134476
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewataka wanafikra na nchi huru duniani kushirikiana katika kukabiliana na ugaidi akisema kuwa sharti la kwanza katika uwanja huo ni kuarifisha ugaidi na kuweka mikakati ya jinsi ya kukabiliana nao.
Rais Ahmadinejad amesema kuwa uungaji mkono wa kimaonyesho wa Marekani kwa haki za mataifa ya Mashariki ya Kati ni kifuniko na mwavuli tu wa kuuokoa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Rais Ahmadinejad ameyasema hayo leo mjini Tehran katika mkutano wa waandishi wa habari wa ndani na nje na kuongeza kuwa baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 Marekani ilileta majeshi yake kwa wingi Mashariki ya Kati kwa ajili ya kudhamini maslahi yake haramu na kuulinda utawala ghasibu wa Israel kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Ameongoza kuwa Washington imebadili siasa zake katika Mashariki ya Kati baada ya harakati za mapinduzi za wananchi japokuwa malengo yake bado ni yale yale ya zamani.
Rais Ahmadinejad amesema serikali ya Marekani inataka kueneza Uislamu wa Kimarekani na Uislamu wa kiliberali ambao unakubaliana na udhibiti wa nchi hiyo na unaokubali kuwepo dola la kikatili na linalopenda kujipanua la Israel katika Mashariki ya Kati. Ametabiri kuwa mabadiliko yaliyotokea kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati yatashuhudiwa pia katika maeneo mengine kama Ulaya na sehemu ya bara Asia.
Kuhusu siasa za Washington nchini Pakistan, Rais wa Iran amesema Tehran ina habari za kuaminika kwamba Marekani ina nia ya kushambulia taasisi za nyuklia za Pakistan na kufanya uharibu katika taasisi hizo kwa lengo la kuidhibiti nchi hiyo na kudhoofisha taifa la serikali ya Islamabad. Ameongeza kuwa kwa njia hiyo, Marekani inataka kutumia fimbo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa kwa ajili ya kutayarisha mpango wa kuingilia zaidi masuala ya ndani ya Pakistan na hatimaye kuidhibiti kikamilifu nchini hiyo. 804844
captcha