IQNA

Kuadhimishwa mwaka wa kuasisiwa Jumuiya ya Kiislamu ya London

13:36 - June 09, 2011
Habari ID: 2135294
Maadhimisho ya mwaka wa 25 wa kuasisiwa Jumuiya ya Kiislamu ya London yalifanyika mjini humo hapo siku ya Jumanne.
Kwa mujibu wa tovuti ya Muhit, viongozi wa nchi kadhaa za Kiafrika, wabunge wa Uingereza, maafisa wa serikali ya nchi hiyo pamoja na mabalozi wa nchi za Kiarabu, Kiafrika na Ulaya walishiriki katika maadhimisho hayo. Maadhimisho hayo yalijumuisha filamu kuhusu shughuli za jumuiya hiyo katika kipindi chote cha miaka 25 iliyopita pamoja na mipango inayotazamiwa kutekelezwa katika siku zijazo. Kuenziwa waanzilishi wa jumuiya hiyo, mashirika na viongozi wa Uingereza wanaoshirikiana nayo katika utekelezaji wa majukumu yake pamoja na wafanyakazi bora wa taasisi hiyo ni miongoni mwa ratiba zilizotekelezwa katika maadhimisho hayo. 805516
captcha