IQNA

Haram ya Imam Hussein (as) kukaribisha makarii mashuhuri wa Qur'an

16:47 - June 14, 2011
Habari ID: 2138316
Haram ya Imam Hussein bin Ali (as) katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq itakaribisha wasomaji mashuhuri wa Qur'ani kutoka maeneo mbalimbali duniani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kituo cha Darul Qur'ani kimeripoti kuwa mahfali hiyo ya Qur'ani ya makarii mashuhuri duniani itafanyika kandokando ya Haram ya mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saw) Imam Hussein (as).
Ijumaa iliyopita pia Darul Qur'ani ya Haram ya Imam Hussein(as) ilitayarisha mahfali ya kiraa ya Qur'ani iliyowashirikisha makarii mashuhuri wa Misri kama Farajullah Shadhli, Abdulfattah al Taruti, Ahmad Ahmad Nueina na Muhammad Abdul Maujud.
Mahfali hiyo ya Qur'ani ilihudhuriwa pia na wasomaji Qur'ani wa Iraq na wafanya ziara katika haram hiyo.
Wasimamizi wa mahfali hiyo ya Qur'ani wamesema kuwa shughuli hiyo ni mwanzo wa hatua mpya za kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Kiislamu kwa ajili ya kutayarisha mahfali za Qur'ani kwa kushirikiana. 808834

captcha