Kwa mujibu wa idara ya uhusiano wa umma ya kituo hicho, maadhimisho hayo ambayo yatahudhuriwa na wapenzi wa Ahlul Beit (as) yamepangwa kuanza saa mbili usiku kwa wakati wa nchi hiyo.
Hujjatul Islam wal Muslimeen Husseini amealikwa kuzungumza katika sherehe hiyo muhimu ya Kiislamu, ambapo atazungumzia shakhsia na matukufu ya Imam Ali (as).
Kituo Cha Kiislamu cha Imam Ali (as) kimewaalika wapenzi na wafuasi wote wa Watu wa Nyumba ya Mtume (saw) kuhudhuria sherehe hiyo. 809280